LICHA ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mdeme kutangaza
kumsimamisha uongozi wa Mwenyekiti wa mtaa wa Malimwa Kusini, Ismail
Seifu (CUF), ametangaza kutokabidhi ofisi ya mtaa kama alivyoagizwa na
DC,
![]() |
Christina Mdeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
|
Seifu amesema kitendo cha mkuu wa wilaya kumsimamisha nafasi hiyo haina
maana yoyote na hatambui suala hilo kwani yeye alichaguliwa na waananchi
na siyo mkuu wa wilaya.
Mkuu wa wilaya aliitisha mkutano wa adhara kwa maelezo kuwa wananchi
walimpelekea tuhuma tano ambazo zilikuwa zikimkabili mwenyekiti huyo
jambo ambalo amesema siyo tuhuma za wananchi bali ni tuhuma za
kutengenezwa kamati yake ya utendaji ambao aliwasimamisha.
Akizungumza na waandishi wa habari Seifu, amesema licha ya mkuu wa
wilaya kufanya utenguzi wa uongozi wake bado hatambui jambo hilo kwani
waotakiwa kumwondoa ni wananchi waliompigia kura.
Seifu amesema wakati wa uongozi wake alihakikisha anapambana katika
kukwamua maendeleo huku akiwa ameokoa zaidi ya Sh milioni nne za mradi
wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF ambazo zilikuwa zikilipwa
katika kaya hewa zaidi ya kumi.
Awali kabla ya kusimamishwa uongozi kwa kutangaziwa tuhuma tano
zilizomkabili Seifu amesema katika uongozi wake hakupendezwa na tabia ya
baadhi ya viongozi kukwamisha maendeleo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa inasikitishwa na tabia ya viongozi hao
kukwamisha maendeleo ya mtaa huo kwa kutosikiliza matatizo ambayo
wanapelekewa.
Amesema licha ya kujitahidi kuhakikisha mtaa huo unapata maendeleo
makubwa lakini bado kuna mambo ambayo viongozi wa Manispaa na wilaya
wanashindwa kuyatolea maamuzi.
Seifu amesema analazimika kusema hivyo kutokana na kuomba wakaguzi wa
milioni kumi ambao ulifanyika huku kukiwa na mapungufu ambayo yanatakiwa
kufanyiwa kazi.
Mwenyekiti huyo amesema mbali na kuomba wakaguzi lakini bado ameweza
kuokoa kiasi cha Sh. milioni nne ambazo zilikuwa zikitolewa katika kaya
masikini kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kaya masikini.
Amesema katika uongozi uliopita zaidi ya kaya kumi katika mtaa wa Mlimwa
Kusini zilikuwa kaya hewa ambazo zilikuwa zikipokea mradi wa TASAF na
taarifa hizo zipo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma pamoja na
ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa lakini hakuna hatua zozote
zilizochukuliwa.
“Mtaa wa Mlimwa kusini hunaongozwa na mwenyekiti kutoka katika muungano
wa vyama vinavyounda Ukawa kupitia CUF ambapo mtaa huo ni makazi ya
Waziri Mkuu.
“Wapo wanasiasa ambao wamekuwa hawataki maendeleo na badala yake
wanaingiza mambo ya siasa katika kazi, mtaa huu unaongozwa na CUF lakini
wapo watu ambao wanatamani kuangusha utawala uliopo,” amesema
mwenyekiti huyo.
Kwa upande wao viongozi wa Manispaa pamoja na wilaya hawakuweza kutoa
ufafanuzi wa jambo lolote kuhusiana na alichokisema mwenyekiti huyo.
Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilimwandikia barua
Kumb.Na.AB.380/507/01/17 ya kumtaka mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma
kutoa taarifa ya ukaguzi uliofanyika katika mtaa wa Mlimwa Kusini.
Post a Comment