0
Ongezeko la watu ikiwemo kambi za wakimbizi katika mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa limechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira na ujangili, hivyo kuathiri uhifadhi wa wanyamapori kama Sokwe, Tembo na wengine katika mikoa hiyo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Jane Good Hall, Emmanuel Mtiti amesema wanyamapori wengi wamekuwa wakikimbia kutokana na ujangili unaofanywa na watu wasio waaminifu na ukataji miti hovyo unaotokana na shughuli za kibinadamu.

Bwana Emmanuel Mtiti alikuwa akizungumza katika majadiliano maalumu jijini Dar es salaam yaliyohusisha Taasisi ya Jane Goodhall inayosimamia uhifadhi wa wanyamapori katika hifadhi ya Gombe na ubalozi wa Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la watu wa Marekani – USAID.

Aidha, Mkurugenzi huyo amewataka wadau mbalimbali wa utalii kushirikiana na Serikali kuboresha miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege ili kurahisisha usafiri kwa watalii wanaofika kwenye hifadhi za wanyamapori.

Post a Comment

 
Top