WATU wawili wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru, Gladys Barthy, kwa tuhuma za kukutwa na kujihusisha na kilimo cha bangi.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni Issa Abdallah (30) na Mariam Rashid (24) ambao wameshtakiwa katika kesi mbili tofauti.
Mwendesha mashtaka, Inspekta Steven Msongaleli, alidai kuwa katika kesi ya kwanza, Abdallah anadaiwa kukutwa na kilo moja na nusu ya bangi pamoja na kilo moja ya mbezi za zao hilo haramu wakati Mariam Rashid (24) aliktwa amepanda miche ya bango katika shamba lenye ukubwa wa ekari moja.
Alidai kuwa Mariam alikamatwa baada ya mume wake ambaye alitambuliwa kwa jina la Mohammed Abdallah kukimbia baada ya kuwaona polisi.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika msako mkali uliofanyika February 18 mwaka huu katika katika mashamba yaliyoko katika Kitongoji cha Mkundi, Kijiji cha Kalulu wilayani Tunduru.
Kwa mujibu wa Msongaleli, watuhumiwa hao walifanya kosa kinyume cha sheria namba 17 kifungu cha (1B na 2) vya kudhibiti madawa ya kulevya namba 5 ya mwaka 2005.
Watuhumiwa wote walikana mashitaka na kesi hizo zitatajwa Machi 5, mwaka huu na upelelezi bado haujakamilika.
Post a Comment