0
LICHA ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewatuliza mashabiki kwa kusema bado wanayo nafasi ya kusonga mbele.

Jumanne wiki hii Yanga ilishindwa kutamba kwenye Uwanja wa Taifa na kufungwa Township Rollers na timu hizo zitarudiana Machi 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Gaborone, Botswana.

Ajibu aliliambia Championi Jumamosi kuwa, bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano hivyo mashabiki wao wasikate tamaa na wawasamehe kwa matokeo mabovu ya awali.

“Bado tunayo nafasi na tunaweza pia nina imani tutawafunga wapinzani wetu nyumbani kwao kikubwa ni kuendelea kutusapoti na sisi tutapambana ili kuweza kupata matokeo.

“Najua mashabiki wetu wameumia kwa matokeo yale, ila hatuna budi kuwaomba msamaha, watusaheme na nafasi ya kufanya vizuri bado tunayo wasikate tamaa,” alisema Ajibu.

Hata hivyo, Yanga ili ifuzu inahitaji ushindi wa uwiano wa mabao 2-0 ili iweze kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama ikitolewa itaangukia katika kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Post a Comment

 
Top