0
Serikali ya Muammar Gaddafi imepoteza euro bilioni 10 katika akaunti za benki zilizohifadhiwa nchini Ubelgiji.

Kulingana na ripoti iliyoandikwa katika gazeti la Belgian Le Vif, ni kwamba fedha hizo zina umuhimu mkubwa kwa serikali ya Libya na kwamba sasa hazipatikani nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa taarigfa ni kwamba kiwango cha Euro bilioni 16 kilihifadhiwa katika akaunti nne tofauti  nje ya Libya mwaka 2011.

Libya ilikuwa miongoni mwa mataifa ambayo yaliuza mafuta kwa kiwango kikubwa mwaka 2011.

Kufuatia azimio la vikwazo vya Umoja wa Mataifa juu ya utawala wa Gaddafi, mali za Libya zenye zaidi ya dola bilioni 60 zilizokuwa katika mataifa mengine Magharibi zilizuiliwa.

Uamuzi wa kuzuiliwa kwa fedha hizo ilikuwa moja ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya serikali ya Libya.

Taarifa zinafahamisha kuwa mwaka 2017 wakati ambazo pesa hizo zilitaka kutaifishwa zilikosekana.

Muammar Gaddafi alikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa ya bara la Afrika ili kufikia malengo ya maendeleo.

Post a Comment

 
Top