0
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa amemwacha nje ya kikosi kiungo wa timu hiyo Paul Pogba ktokana na kuumia kwenmye mazoezi ya jana hivyo asingeweza kumchezesha akiwa majeruhi.

"Aliumia jana kwenye mazoezi na alikuwa na hali mbaya hovyo lazima akae nje kutokana na maumivu makali aliyonayo'', amesema Mourinho kwenye mahojiano na wanahabari muda mfupi kabla ya mechi ya leo kuanza dhidi ya Livewrpool.

Hata hivyo Mourinho amekataa kuweka wazi kuwa ni tataizo gani haswa linamsumbua Pogba huku pia akigoma kueleza nyoa huyo raia wa Ufaransa atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.

Pogba hajawa na mwendelezo mzuri wa kucheza baada ya kutolewa kwenye mchezo dhidi ya Tottenham pamoja na ule wa Newcastle United mwezi Februari huku pia akiwekwa nje kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa mechi ya kwanza ya 16 bora dhidi ya Sevilla.

Mlinzi Eric Bailly ameanza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu mwezi Novemba akikaa nje kwa  miezi mitatu kutokana na kusumbuliwa na mejeraha ya goti.

Post a Comment

 
Top