0
Askari na maafisa wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma leo wamefanya zoezi la utayari huku ,viongozi wa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama wakitoa onyo kwa yeyote atakayetaka kuharibu hali ya utulivu na amani iliyopo mkoani humo.

Wakati wa zoezi hilo la utayari askari na maafisa hao wakiwa wamevalia sare zao rasmi za kazi kasoro wale wa idara ya usalama wa taifa walipita katika mitaa mbalimbali ya mkoa wa dodoma tangu majira ya saa kumi na moja asubuhi hadi majira ya saa nne na kuhitimisha zoezi hilo la utayari katika uwanja wa Jamhuri.

Akizungumza kwenye uwanja huo wa Jamhuri,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Dodoma ambaye ni mkuu wa mkoa huo Dkt.Binilith Mahenge amewaagiza maaskari na maafisa hao kwa ushirikiano waliouonyesha katika zoezi hilo la utayari waendelee nao kuhakikisha Dodoma inakuwa shwari.

Viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Dodoma wamesema vikosi wanavyoviongoza vipo sawa kukabiliana na jambo lolote baya litakalotokea mkoani Dodoma na wamewaonya watu ambao wanafikiria kufanya jambo ovu mkoani humo kuwa watajutia vitendo vyao.

Post a Comment

 
Top