0
Wananchi katika kata ya mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamewalalamikia baadhi ya walimu kwa kutoa adhabu kali zilizopitiliza kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hatua inayosababisha baadhi yao kuacha shule na kukimbia  shule ni mahali pa mateso.

Malalamiko hayo yanatolewa Bi. Rehema Bula mzazi wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mchoteka  Mohamhamed Kaissy amekimbia shuleni na nyumbani na hajulikani aliko hadi sasa ambapo wakati mama yake huyo akimpeleka shule alimhoji anataka afe baada ya kuona wenzake wakipanga mstari na kuchapwa viboko na kuamua kukimbia.

Akijibu kero hiyo mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Juma Homera amewataka walimu wilayani humo kuacha kutoa adhabu zilizopitiliza kwa wanafunzi na kuagiza wanafunzi waliokimbia shule kukimbia adhabu kurejea shuleni haraka kuendelea na masomo.

Post a Comment

 
Top