0
James Timber, Kwimba
Afisa ustawi wa jamii katika wilaya Kwimba mkoani Mwanza Bw. Salumu Liundu amepongeza mradi wa watu wasioona (TLB) baada ya kikao cha tathminini robo ya mwaka kuonesha wamepunguza umasikini wa kijamii kwa kuanzisha vikundi vya ujasiamali.

Bw. Liundu alisema kuwa mradi huo umepokelewa vizuri na jamii hasa suala la maendeleo limekuwa limepiga hatua kwa kiasi kikubwa tofauti na hapo awali ambapo jamii ilikuwa haitoi ushirikiano na mradi na wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu.

“Nashangaa jamii na wazazi hawakuwa tayri kutoa ushirikiano katika mradi huu walikuwa wanawaficha watoto walemavu wasijulikane, jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya baadaye wanapokuwa,” alisema.

Bi.Mariam John ni moja kati ya watu walionufaika na mradi huo alisema kuwa changamoto awali jamii haikutambua wala kujali na kuthamini mradi huo na kuwa na mtazamo hasi, jambo lililochelewesha mafanikio, japo kwa sasa wamepokea vizuri na amepanda kiuchumi kutokana na shughuli wanazofanya.

“Nilipoingia kwenye vikundi vilivyoanzishwa na mradi huu tulikuwa wachache ila na kipato kilikuwa kidogo, kwa sasa wameongezeka na kipato kimepanda kutokana na uzalishaji umeongezeka,” alisema Bi. John.

Naye Afisa Elimu Kitengo Maaluum wilayani hapo Bi. Elizabeth Tenga  alisema kuwa amekuwa akishirikiana na mradi huo kwenye suala la utetezi na ushawishi ili kupata haki za walemavu katika kata 10 na matokeo yamekuwa safi kwani jamii na wazazi wameelewa.

Bi. Tenga alisema kuwa mikakati walionayo mradi huo ni kuwaomba halmashauri na taasisi binafsi kutengeneza miundombinu rafiki kwa walemevu waendapo kupata huduma katika majengo hayo.

“Wito wangu ni kwa taasisi na serikali kujenga majengo yenye miundombinu rafiki kwa ajili ya walemavu iwe rahisi kufika na kupata huduma kwa wepesi kwani itachangia kupunguza changamoto kwa walemavu,” alisema.

Post a Comment

 
Top