0
Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT)kwa kauli moja wamempongeza Rais John Magufuli kwa kauli yake ya kuzuia maandamano nchini na kusisitiza wanawake wa Tanzania hawapo tayari kuandamana.

Pia wamempongeza Rais Magufuli na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein kwa usimamizi mzuri wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwani wamefanikisha uchumi wa Tanzania kuimarika.Pamoja na hayo Kamati hiyo imetangaza kuanza kazi rasmi za UWT ambapo kati ya vipaumbele ambavyo wamepanga kuvifanya kwa kipindi cha miaka mitano ni 18 lakini wametangaza na vipaumbele vinne.

Hayo yamesemwa leo jijini  Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka wakati akitangaza maazimio ya kikao cha Kamati ya Baraza Kuu la jumuiya hiyo.

Aidha akizungumzia kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia maandamano nchini,Kabaka amesema wanaukanga mkono kauli hiyo na kusisitiza kuwa wanawake wa Tanzania hawapo tayari kushiriki kwenye kufanya maandamano.

Amesema kuwa jukumu la wanawake wa Tanzania ni kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kimaendeleo na kwamba wanalaani kauli za baadhi ya viongozi na watu wengine ambao wamekuwa wakitoa lugha zinazoashiria uvunjifu wa amani nchini.

"Tunaomba viongizi wa dini na viongozi wa kimila kuhakikisha wanatoa kauli za kujenga na kuhamasisha umoja,amani ,upendo ,heshima na mshikamano." Tunampongeza Rais Magufuli na Rais Shein kwa kuendelea kukemea watu wasiotakia nchi yetu iwe na amani kwa kutaka kufanya maandamano au matamko ya uchochezi,"amesema Kabaka.

Ameongeza kuwa "Watanzania hatuna muda wa maandamano ,tuna muda wa kufanya kazi ili kujiletea maendeleo ya nchi yetu tajiri,"amesema.

Post a Comment

 
Top