0

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limehitimisha mkutano wake wa 11 wa bunge la bajeti baada ya kukamilisha shughuli zote zilizopangwa kufanyika ikiwemo kupitishwa bajeti za wizara 21 na bajeti kuu ya serikali 2018/19.

Akitoa hoja ya kuhairisha bunge Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelihakikishia bunge kuwa serikali itazingatia ushauri na maoni yaliyotolewa kuhakikisha wanasimamia na kuweka nidhamu katika matumizi ya fedha kama ilivyopangwa huku akiziagiza taasisi kusimamia miradi ikamilike kwa wakati ili kuleta maendeleo nchini.

Aidha amewataka watumishi wote wanaohusika katika kukusanya mapato kuhakikisha wanakusanya mapato ipasavyo ili kuwezesha utekelezaji wa bajeti na matumizi ya mashine za Kielectroniki za ukusanyaji wa mapato EFD ili kuepusha upotevu wa aina yoyote.

Kuhusu sekta ya Kilimo Waziri Mkuu MAJALIWA amesema serikali itaendelea kusimamia ukuzaji na uendelezaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Mkonge, Tumbaku, Kahawa, Korosho ambayo serikali imejiwekea mikakati na utoaji wa pembejeo kwa wakulima ili kukuza sekta ya kilimo nchini na kuleta tija ikiwemo utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo ya sekta ya kilimo uliozinduliwa hivi karibuni na mh rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza kabla ya kuhairisha Bunge Spika wa bunge Job Ndugai ameiambia serikali, kama bunge wanategemea yaliyoamuliwa yatafanyiwa kazi na bunge limehairishwa mpaka septemba 4 mwaka 2018.

Post a Comment

 
Top