0

Viongozi wa Ethiopia na Eritrea wamekubaliana kukutana kwa mara ya kwanza katika muda wa takribani miaka 20 ishara ambayo haikutegemewa ya kuanza upya uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili jirani kwenye pembe ya Afrika.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, Workneh Gebeyehu aliliambia shirika la habari la Associated Press-AP siku ya Alhamis kwamba mkutano huo utajenga msingi bora wa kurejesha amani. Aliongeza kuwa muda na mahala ambako mkutano utafanyika bado haujajulikana.

Mwanadiplomasia wa juu wa Ethiopia alizungumza wakati ujumbe wa Eritrea ulio-ongozwa na waziri wa mambo ya nje, Osman Saleh kumaliza ziara ya siku tatu ya kihistoria huko Ethiopia.

Mahusiano mabaya ya nchi hizo mbili yalianza wakati vita vya mpaka vilipotokea mwaka 1998 miaka mitano baada ya Eritrea ilipojinyakulia uhuru wake kutoka Ethiopia.

Post a Comment

 
Top