0

Kiungo wa klabu ya Manchester United, Marouane Fellaini ameongeza kandarasi yake ndani ya timu hiyo itakayomfanya kuendelea kusalia hapo mpaka mwezi Juni mwaka 2020.

Nyota huyo ambaye alijunga na klabu hiyo akitokea Everton kipindi cha kocha David Moyes amekuwa akishutumiwa na mashabiki na wakongwe wa United kutokana na kiwango chake.

Fellaini ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi ametoa habari hiyo kuwa ataendelea na mashetani hao wekundu wa Uingereza.

“Ningependa kuwataarifu kuwa nitaendelea kuwa mchezaji wa Manchester United, nimefanya maamuzi haya kwakuwa najisikia furaha kuwa hapa,” amesema Fellaini.

Mchezaji huyo pia ameongeza kuwa “Ninajiskia kuwa miongoni mwa hii timu hasa chini ya uongozi wa Jose bado tunamengi tunayo hitaji kuyafikia. Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwako Jose kwa mapenzi yako sikuzote unayoonyesha kwangu.”

Meneja wa United, Jose Mourinho amesema kuwa anajiskia mwenye furaha baada ya kuona Marouane anaendelea kusalia kwakuwa anaamini siku zote vile anavyotamani kuendelea kuwepo ndani ya klabu.

Post a Comment

 
Top