0

 


Katika taarifa yake ya sasa Ikulu ya Marekani imesema Rais Joe Biden leo hii atatembelea mji wa Poland ambao uko karibu na mpaka na Ukraine, kwa lengo la kuonesha mshikamano na Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.Katika eneo hilo la Rzesow, lililo umbali wa kilometa 50 kutoka mpakani mwa Ukraine, Biden atakutana na Rais wa Poland, Andrzej Duda. 


Ni sehemu ya safari yake ya dharura barani Ulaya ambayo imesababisha na vita vya Ukraine.Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika ziara yake ya Machi 5 alilitembelea eneo hilo kwa lengo la kuonesha uungwaji wake mkono kwa wanajeshi wa NATO, la iliyokuwa sehemu ya Jumuiya ya Kisovieti.


Ikulu ya Marekani inasema katika ziara hiyo ya Ijumaa hii pia, Biden atapokea taarifa ya namna gani Poland inakabiliana na wimbi la mamilioni ya wakimbizi ambao wanakimbia makombora ya Urusi huko Ukraine. Aidha atakutana na wanajeshi wa kikosi cha anga ambao wana kambi yao katika eneo hilo la Rzeszw

Post a Comment

 
Top