0

 


Kiongozi wa kundi linalopinga wahamiaji nchini Afrika Kusini alikamatwa siku ya Alhamisi, vyombo vya habari nchini humo vinaripoti.


Nhlanhla Lux Dlamini, 33, ameripotiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi katika mji mkuu wa kibiashara wa Johannesburg.


Sababu ya kukamatwa kwake hazijabainika


Kindi lake, Operation Dudula, limekuwa likifanya kampeni dhidi ya raia wa kigeni wasio na vibali nchini.


Uungwaji mkono wa kundi hilo umekuwa ukiongezeka miongoni mwa jamii ya Wafrika Kusini wanaohisi kutengwa.


Kuna wasiwasi kwamba kampeni zake zinaweza kusababisha kuzuka tena kwa ghasia za chuki dhidi ya wageni nchini.

Post a Comment

 
Top