
Septemba 30 2016 wakala wa mchezaji ghali zaidi duniani Mino Raiola ameweka wazi kwa nini kocha wa Man United Jose Mourinho alishindwa kumsajili Paul Pogba wakati akiwa Chelsea, Raiola ameweka wazi kuwa Mourinho ni miongoni mwa makocha waliokuwa wanamuhitaji Pogba kwa muda mrefu.
Raiola ameeleza kuwa kilichomfanya Jose Mourinho amkose Paul Pogba akiwa Chelsea, kwa sababu alikuwa na makubaliano maalum na klabu ya Juventus kuhusu kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Raiola alikuwa ameshaubaliana na Juventus kuwa Pogba aisaidie timu hiyo kutwaa taji la Serie A na UEFA Champions League ndio aondoke.

Mino Raiola
“Pogba
angeweza kuondoka Juventus mwaka uliopita kwa sababu Jose Mourinho
alimuhitaji wakati yupo Chelsea, kiukweli alimuhitaji sana lakini
Juventus na mimi tulikuwa na makubaliano kuwa aisaidie timu kutwaa taji
la Serie A na Champions League kwanza ndio angeweza kuruhusiwa kuondoka”
>>>> Raiola
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.