0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanaotaka kuzichukua klabu za Yanga na Simba kuiga mfano wa Azam FC kuunda timu zao.
Makonda aliyasema hayo alipotembelea maskani ya klabu ya Azam FC huko Chamazi, Mbagala wakati wa ziara yake katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam akiwa na lengo ya kuipongeza kwa juhudi zake.
Alitoa mwito kwa watu wengine wenye uwezo kujitokeza, na kuiga mfano wa watu wa Azam FC ili kuwa na timu nyingi zenye ushindani na kuondoa migogoro kwenye soka la Tanzania.
mohamed-dewji-yusuph-manji-simba-yanga
“Waige mfano wa Azam, watengeneze timu zao, watengeneze viwanja ili tuwe na watu wengi, tuwe na timu nyingi zenye ushindani na hata hii migogoro inayotokea Yanga na Simba haitakuwepo”, alisema.
Aliwataka wenye fedha zao kutohangaika na kama wamegomewa kukodishwa waje tu watengeneze timu zao ili na wenyewe waendelee kunufaika kwa sababu mwisho wa siku timuhizop zitasaidia. Alisema kuwa kukiwa na timu nyingi vijana watapata sehemu za kufanyia kazi na kupunguza watu wanahangaika mitaani bila ya kazi.
“Na hivyo ndivyo tunaweza kuweka vijana wengi wakawa kwenye vipaji vyao tukajenga uchumi wetu kupitia ajira inayotokana na michezo na mwisho wa siku tukapeperusha vema bendera ya Taifa letu katika mataifa mbalimbali katika sekta nzima ya michezo,”alisema.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Azam FC, alimshukuru Makonda kwa ugeni wake huo ndani ya klabu hiyo, huku akichukua fursa hiyo pia kumwelezea historia fupi ya Azam tokea ianzishwe mwaka 2004 hadi ilipo mpaka sasa.
Aliongeza kuwa: “Kwa hiyo sisi tunaamini ya kuwa hata Mheshimiwa hapa Mkuu wa Mkoa utakuwa ni miongoni mwa wadau wetu wakubwa wa kutusapoti na karibu sana Azam FC usichoke kuja wakati wowote.”

Post a Comment

 
Top