Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepiga marufuku wauzaji holela
wa samaki na mboga mitaani badala yake wapeleke katika masoko maalumu.
Aidha ameliagiza jeshi la polisi na halmashauri zote mkoani humu kuwakamata wafanyabiashara watakaokiuka agizo hilo.
Makonda
alitoa kauli hiyo jana, wakati alipotembelea Soko la Kimataifa la
Samaki la Feri na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo, ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika Wilaya ya Ilala.
Wafanyabiashara
hao walieleza kuwa, moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na
kuzagaa kwa wafanyabiashara huria wa samaki hususani katika vituo vya
mabasi ya daladala na pembezoni mwa barabara mkoani humo.
Walidai
kuwa, hali hiyo inahatarisha uhai wa soko hilo kwani watu wengi
hawafiki kununua samaki katika soko hilo, badala yake huishia kununua
katika vituo vya mabasi na mitaani.
Mfanyabiashara
Said Ally alimueleza mkuu huyo wa mkoa kuwa, masoko huria ya mitaani
yanaendelea kushamiri huku viongozi wa halmashauri na wananchi wakikaa
kimya.
“Mkuu
wa mkoa tusaidie sasa hivi kila kona kuna wauza samaki hasa katika
vituo vya mabasi jambo linalosababisha feri tunakosa wateja wanaishia
mtaani, soko litakufa kwa sababu watu hawaji tena tofauti na awali,” alisema Ngasa.
Mbali
na hayo wafanyabiashara hao waliomba kuboreshwa kwa miundombinu ya soko
hilo ambayo imechakaa licha ya soko kuwa la kimtaifa.
Kutokana
na malalamiko hayo, Makonda alipiga marufuku biashara ya samaki na
mboga mitaani na kumuagiza Kamanda wa Operesheni, Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Lucas Mkondya kuwashughulikia wafanyabiashara wote watakao
kiuka agizo hilo kuanzia sasa.
“Ni
marufuku kufanya biashara ya samaki na mboga katika maeneo ambayo sio
rasmi wafanyabiashara wapeleke katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya
kufanyia biashara hizo,” alisema Makonda.
Post a Comment