![]() |
Komando William Ryan Owen wa jeshi la wanamaji la Marekani |
Baba ya mwanamaji wa Marekani aliyeuawa katika uvamizi wa wapiganaji wa
al Qaeda mjini Yemen mwezi uliopita amesema kuwa alikataa kukutana na
rais wa Marekani Donald Trump wakati mwili wa mwanaye ulipowasili
Marekani.
''Sitaki kumuona alimwambia kiongozi mmoja wa dini wakati huo''.
Shambulio hilo la tarehe 28 mwezi Januari lilikuwa la kwanza lililoagizwa na Bwana Trump.
Bill Owens ambaye mwanawe William Ryan Owen aliuawa, aliambia jarida la
Miami Herald kwamba serikali inafaa kumfanyia uchunguzi mwanawe.
''Kwa nini kuwepo kwa ujumbe kama huo wiki moja baada ya yeye kuchukua
mamlaka. Kwa nini''? Alisema katika mahojiano na gazeti hilo.
''Kwa kipindi cha miaka miwili hakuna mwanajeshi aliyeruhusiwa kuelekea
Yemen, walikuwa wakitumia makombora na ndege zisozokuwa na rubani
kutekeleza mashambulio kwa sababu hakukuwa na raia yeyote wa Marekani
aliyekuwa akilengwa. Sasa mara moja tunachukua hatua hii''.
Uvamizi huo ulioagizwa na rais Trump siku sita baada ya kuchukua mamlaka unaaminika kuwaua raia kadhaa ikiwemo watoto.
Wamarekani 3 walijeruhiwa katika uvamizi huo uliodaiwa kuanza kupangwa na utawala wa rais Obama.
Post a Comment