0
picha: Maktaba
Dar es Salaam. Katika kuonyesha wamedhamiria, mashabiki wa Simba walianza kuingia uwanjani saa tano asubuhi kusubiri mchezo dhidi ya watani zao Yanga utakaoanza saa 10:00 jioni.

Mashabiki hao walifika uwanjani wengi wao walipitiliza moja kwa moja majukwaani huku upande wa Yanga msururu wa kuingia uwanjani ukiwa bado haijachanganya.

Upekuzi hadi kwenye pochi

Achilia mbali vikosi vya mbwa na farasi, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, askari wa magetini wameimarisha usalama kwa kufanya upekuzi hadi kwenye pochi za kutunzia fedha.

Yanga, Simba wacheza Singeli pamoja

Ili kuonyesha shamra shamra ya mchezo huo, mashabiki kadhaa wa Simba na Yanga waliamua kusimama kwa muda katoka barabara kuu ya Veta na kuanza kucheza singeli.

Mashabiki hao waliokkuwa wamevaa jezi za njano na nyekundu walionyesha umahiri wao wa kucheza muziki huo huku baadhi yao wakipiga mavuvuzela na kuimba nyimbo za kejeli kwa timu pinzani.

Yanga yawambia Simba wasing'oe viti

Mashabiki wa Yanga wa tawi la Keko Furniture wamewakebehi wale wa Simba wakiwa njiani kuelekea taifa na kuwaonya kutong'oa viti.

"Leo mking'oa viti mjue ni moja kwa moja mnapelekwa jela, sasa nendeni mkafanye vurugu huku, mabomu mtapigwa, mtafungwa na jela mtakwenda," alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Musa Peter.

Post a Comment

 
Top