0

Wafanyakazi 14 wa Kampuni ya Quality Group Ltd wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi viza za biashara, kuishi na kufanya kazi nchini bila vibali
Waliofikishwa mahakamani ni Meneja msaidizi, mhasibu na washauri 12.
Akiwasomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma alidai washtakiwa kwa pamoja Februari 13, katika Kampuni ya Quality Group Ltd iliyopo wilayani Ilala, wakiwa raia wa India walikamatwa wakiwa na viza za biashara zilizoghushiwa, wakiishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria.
Washtakiwa walikana mashtaka na ilielezwa upelelezi wa kesi umekamilika.
Hakimu Mkeha alimtaka kila mshtakiwa kusaini bondi ya Sh5 milioni. Washtakiwa hao wanaotetewa na mawakili Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, watasomewa maelezo ya awali Machi 7 wote wapo nje kwa dhamana

Post a Comment

 
Top