Tume maalum iliyoundwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa kwa ajili ya
uchunguzi kuhusiana na sakata la mnyama Faru John imekabidhi taarifa ya
uchunguzi wa ripoti hiyo ambapo imethibitisha kifo cha Mnyama huyo na
kutoa mapendekezo ya kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa uongozi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Akikabidhi taarifa hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samweli Manyele amesema kupitia sampuli 45 ikiwemo sampuli za mifupa, Pembe Damu na Ngozi ambazo zilifanyiwa uchunguzi katika chuo kikuu cha Pritoria cha Afrika Kusini Zilithibitisha kwa asilimia 100 kuwa sampuli hizo zinafanana na vinasaba vya mnyama faru John.
Taarifa hiyo pia ilieleza kifo cha mnyama Faru John kilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutelekezwa na idara ya hifadhi ya wanyama pori pamoja na uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro NCAA ambapo kwa kushirikiana na wamiliki wa hifadhi ya Gurunet walishindwa kutoa matibabu kwa mnyama huyo na kupelekea kifo chake.
Aidha kwa kushirikiana na taasisi za serikali zinazojihusisha na makosa ya jinai ilibaini uwepo wa ukiukwaji wa taratibu na sheria mbalimbali za nchi ikiwemo kutokuwepo kwa kumbukumbu rasmi za uhamisho wa Faru John Kuelekea hifadhi binafsi ya Guruneti huku ikibainika kuwepo kwa maslahi binafsi kwa watu walioshiriki kumuhamisha mnyama huyo.
Akipokea taarifa hiyo ambayo ilianza kufanyiwa uchunguzi tangu Desemba 10 mwaka jana Waziri mkuu Majaliwa amesema kwa sasa Serikali inaipitia kwa umakini huku ikitarajia kutoa msimamo wake hivi karibuni kwa kuzingatia mapendekezo ya tume hiyo ambapo pia ilishauri kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa baadhi ya viongozi wa wa wizara waliojaribu kukwamisha uchunguzi.

Post a Comment