Baada ya taarifa ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge chini
ya mtani na kaka yangu Kepteni Mstaafu George Huruma Mkuchika
kukabidhiwa kwa Spika, Spika ataiweka taarifa hiyo katika ratiba za
shughuli za Bunge ili iwasilishwe na kujadiliwa. Tayari Mkuchika na
Kamati yake wameshakamilisha taarifa yao tayari kuikabidhi kwa Spika,
Ndugu Job Justino Ndugai.
Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa kati ya leo au
kesho. Taarifa ya Kamati ya Mkuchika itabeba kilichopatika katika
mahojiano na Makonda; maoni na mapendekezo ya Kamati. Makonda (Daudi
Albert Bashite) aliitwa kuhojiwa na Bunge kupitia Kamati hiyo kwa
kulidharau Bunge kupitia kauli zake za kejeli na kiburi alizozitoa juu
ya Bunge na Wabunge.
Katika hali ya 'kudhibiti' kauli na mwenendo wa Wabunge wa CCM kuhusu
taarifa hiyo, viongozi wa Wabunge wa CCM wameanza kuwapanga Wabunge wa
CCM. Kuwapanga huko kunaratibiwa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Ndugu
Jason Rweikiza. Rweikiza, kwa mujibu wa taarifa toka Dodoma, anawataka
Wabunge kupongeza hatua ya Makonda ya kuomba msamaha kwa barua.
Imeelekezwa kuwa kama Rweikiza na timu yake watakwama kuwapanga Wabunge
wa CCM kuhusu taarifa hiyo, basi kutalazimu kuwepo kwa Kikao cha Wabunge
wote wa CCM almaarufu kama Party Caucus ili Wabunge waandaliwe na
utaratibu wa kuwamulika mjadala utakapoanza uwekwe. Maandalizi ya haraka
ya Caucus yatafanyika.
Post a Comment