Liverpool na Arsenal zimeingia vitani kuwania saini ya mchezaji wa AS Monaco, Thomas Lemar mwishoni wa msimu huu.
Taarifa zinaweka wazi kwamba makocha wa timu hizo mbili, Jurgen Klopp na
Arsene Wenger wote wana fedha za kufanya usajili wakati dirisha la
majira ya kiangazi litakapofunguliwa na kwamba, kila mmoja ametenga
Pauni 90 milioni kuinasa huduma ya staa huyo wa Ufaransa.
Liverpool na Arsenal zote zimeondokewa na mastaa wake wa maana katika
dirisha hili la usajili, ambapo Philippe Coutinho ameachana na wababe
hao wa Anfield akitimkia Barcelona, wakati Alexis Sanchez aliondoka
Emirates kwenda Manchester United. Kuna mastaa wengi wanaosakwa na
makocha hao, lakini vita inaripotiwa kwamba, itakuwa kali kwelikweli kwa
Lemar.
Hata hivyo, Arsenal na Liverpool si wao tu watakaoitaka huduma ya Lemar
baada ya Manchester City nao kutajwa kwenye vita kutokana na kumkosa
Sanchez, huku matajiri wa Paris, PSG wakimweka kwenye mipango yao ya
msimu ujao Mfaransa huyo.
Wenger alikaribia kumnasa Lemar katika dirisha lililopita baada ya
kukubali kulipa Pauni 92 milioni, lakini staa huyo mwenyewe aligoma
kuihama Monaco katika dakika za mwisho na kubaki katika timu hiyo ya
huko kwenye Ligue 1.
Post a Comment