Polisi mjini Tanga jana walilazimika kuingilia na kuzima vurugu zilizotokea katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Tanga zilizotokana na madiwani kugawanyika katika makundi mawili.
Makundi
hayo ya madiwani yaligawanyika kuhusu uamuzi wa wenzao waliohudhuria
kikao cha baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12.
Vurugu
zilianza baada ya Mwenyekiti wa CUF wilayani humo, Rashid Jumbe ambaye
pia ni diwani wa Mwanzage aliyegombea nafasi ya umeya kuamuru madiwani
waliohudhuria baraza hilo watoke nje ili wajumbe waanze kumjadili mmoja
mmoja.
Baada
ya amri hiyo kundi la madiwani 12 waliotolewa nje kusubiri kuhojiwa
waliamua kuingia kwa nguvu kutaka kumtoa Jumbe wakidai anasababisha
makundi ndani ya chama hicho.
Vurugu
ziliendelea kwenye mlango wa kuingilia, jambo lililosababisha wanachama
waliokuwa nje kuingilia kati, huku wakirushiana ngumi.
Baadaye
magari matatu ya polisi yaliwasili katika ofisi hizo na kuwatawanya
wanachama waliokuwa wamejaa, jambo lililomsaidia Jumbe kufanikiwa
kutoka.
Akizungumza
baada ya vurugu hizo, Jumbe alisema kikao hicho kilikuwa na ajenda ya
kuwahoji na kisha kuwajadili madiwani waliohudhuria baraza hilo kinyume
na msimamo wa CUF.
Katibu
wa CUF wa wilaya hiyo, Thobias Haule ambaye pia ni diwani wa Mnyanjani
alisema madiwani waliohudhuria kikao cha baraza hawakwenda kinyume na
chama kwa sababu waliamua kuwawakilisha wananchi waliowachagua, badala
ya kuendeleza mgomo ambao hauwasaidii.
“Tukubali
kwamba kwa kipindi cha mwaka mmoja tulichokaa bila kushiriki vikao vya
baraza kuna mambo mengi ya maendeleo ya wananchi ambayo hayakufanyika,
tumeamua kuhudhuria kwa masilahi mapana ya wananchi,” alisema Haule.
Mbunge
wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk aliwataka wanachama wao kuwa wavumilivu
kwa viongozi wako imara na hawatakubali kuyumbishwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema Jumbe alifikishwa
Kituo cha Polisi Chumbageni kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Halmashauri ya
Jiji la Tanga ina jumla ya madiwani 36; CUF inao 20 na CCM wako 16.
Post a Comment