Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua
Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2016.
Prof.
Ninatubu Mbora Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi
Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia tarehe 20 Agosti, 2015.
Prof.
Ninatubu Mbora Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (Associate Professor of Construction Management –
University of Dar es Salaam).
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Oktoba, 2016
Post a Comment