Wanafunzi
wa kike 12 wanaosoma Shule ya Msingi Nditi, Wilaya ya Nachingwea,
mkoani Lindi, wamekumbwa na ugonjwa wa kuanguka ghafla na wengine
kupoteza fahamu, walipokuwa wakicheza katika viwanja vya shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amon Livigha, alikiri kutokea tukio hilo katikati ya wiki iliyopita, saa mbili asubuhi.
Alisema baada ya tukio hilo, baadhi ya wazazi walifika shuleni hapo na kuwachukua watoto wao na kwenda nao nyumbani.
“Nilipata
taarifa ya kuanguka kwa wanafunzi hao nikiwa darasani nafundisha, hivyo
kutokana na uzito wa tatizo, nililazimika kukatisha masomo na kwenda
kuwahudumia watoto hao.
“Wakati
tukiendelea kufanya utaratibu wa kuwakimbiza wanafunzi hao kituo cha
afya kupatiwa huduma, baadhi ya wazazi walikataa watoto wao wasipelekwe
hospitali na kuondoka nao,” alisema.
Mwalimu
Livigha alisema kutokana na tukio hilo, kamati ya shule, wazazi na
uongozi wa Serikali ya kijiji na kata hiyo wamekutana kujadili suala
hilo.
Mtendaji
wa kata hiyo, Juma Mng’anga, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kuwa
tayari wameshatoa taarifa makao makuu ya wilaya, Nachingwea.
Post a Comment