0
NA MAREGES NYAMAKA,
BAADA timu ya Azam FC kushindwa kupata ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya African Lyon, mchezo wa awali wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivi sasa timu hiyo inaelekeza nguvu zake na kila aina ya mbinu kwenye mchezo wao dhidi ya Majimaji ya Songea.
Akizungumza na DIMBA Jumatano  jana, Meneja wa kikosi hicho, Philipo Alando, alisema kocha anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita akiamini watafanya vizuri dhidi ya Majimaji.
“Tunaamini tunakwenda kuchukua pointi zote tatu mjini Songea, mbele ya Majimaji, hasa baada ya kocha kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa awali dhidi ya African Lyon.
Huku Azam wakieleza tambo zao, naye Kocha Mkuu wa Majimaji, Kali Ongala, alisema ni wakati wa kulipa kisasi kwa timu yake kutumia vema uwanja wake wa nyumbani kuhakikisha anapata ushindi.
“Azam ni timu nzuri, tunaiheshimu, lakini niseme wazi kwamba hatutaruhusu kupoteza kiwepesi kwenye uwanja wetu wa nyumbani, kwani wao kwenye mchezo wa kwanza walitumia uwanja wao wa Azam Complex kupata pointi tatu na sisi ni zamu yetu kutumia Uwanja wa Majimaji kupata pointi,” alisema Ongala, raia wa Uingereza.
Katika mzunguko wa kwanza, timu hizo zilipokutana Uwanja wa Chamazi Complex, Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji, ikiwa chini ya Kocha Peter Mhina.

Post a Comment

 
Top