NA SAADA SALIM,
BAADA ya beki wa Simba, Abdi Banda kuonyesha kiwango kizuri katika michezo mitatu aliyopewa, Kocha wa kikosi hicho, Joseph Omog, amemsifia na kupongeza jitihada alizozionyesha nyota huyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
Omog ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, Banda alionyesha kiwango cha juu, lakini akiwapongeza wachezaji wengine kwenye kikosi hicho ambao wamefanya kazi kubwa.
“Hakuna mechi rahisi, kila mtu anatakiwa apambane kupata ushindi kulingana na majukumu ambayo anapewa katika timu.”
Omog alisema kwa sasa nguvu na akili zake wanazielekeza katika mchezo wao ujao dhidi ya JKT Ruvu, ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza walilazimishwa sare.
Simba ilianza vyema katika mzunguko wa pili baada ya kupata ushindi wa mabao mabao 3-0 ilipokutana na Ndanda FC, matokeo yaliyowafanya kuendekea kubakia kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 38, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 36.
Banda hakuwapo kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa beki raia wa Uganda, Jjuuko Murshid pamoja na Novarty Lufunga, ambapo sasa amepewa nafasi ya kuitendea haki.

Post a Comment