ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam Dkt. Valentine Mokiwa amesema
kuwa yeye anatambua bado ni ndiye askofu wa Dar na hakuna mtu wa
kumfukuza bali mtu wa kumfuta kazi ni Sinodi ya Dar, Kanisa la Anglikana
lina kanuni na taratibu zake wala sio askofu mkuu au askofu mwingine
yeyote wa kanisa la Anglikana Tanzania.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na vyombo vya
habari baada ya tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi yake yanayodaiwa
kufunguliwa na walei 32 (waumini) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar
es Salaam yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya ndiye
anayedaiwa kumvua uaskofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
Dkt. Mokiwa amesema kuwa tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake ni za
kumchafua na kulenga kumchonganisha dhidi ya waumini wake na wanaofanya
hivyo ni wale waliokiuka miiko ya kanisa akawavua vyeo, huku akiwataja
kuwa ni Mchungaji John Mhina, mchungaji Johnson Chinyong’ole wa kanisa
la Newala na Paul Mtweve aliyemtaja kuwa alikuwa katibu wa uinjilisti
Dayosisi ya Magomeni.
Alisema kuwa hao ndio wavunjifu wa amani katika dayosisi hiyo ndio maana
akaamua kuwatimua na hivi sasa wamerudi kivingine ndio hao hao ambao
wamesababisha mgogoro huu unaojitokeza hivi sasa.
Dk. Mokiwa alisema kuwa alishangazwa, askofu mkuu Dk. Chimeledya na
ujumbe wake kuhudhuria kikao cha hivi karibuni cha Halmashauri ya kudumu
ya dayosisi ya Dar es Salaam na kutangaza uamuzi wa kumvua uaskofu tena
kukiwa na ulinzi wa polisi kinyume na utaratibu wa kanisa kuja na
askali kanisani.
“Mwenye mamlaka ya kunifukuza kazi ni yule aliyeniajiri, na mwajiri wangu ni Sinodi ya Dar es Salaam na wote wanasambaza habari hizi za uchochezi ni wale niliowavulisha madaraka ya kuwa viongozi. alisema
Mwandishi wa mtandao huu, Denis Mtima akimpa tuhuma zake mchungaji, John
Mhina wa kainisa la magomeni zilizotolewa na Askofu Mokiwa.
Alisema waraka ambao umesambazwa na askofu mkuu wa Tanzania haujapitia
kwenye halmashauri ya kudumu ya dayosisi ili kupata baraka zake na wala
hauna baraka kutoka kwa sinodi ya dayosisi jambo ambalo linaufanya
waraka huo ukose sifa za kutekelezeka.
“Ninachowaambia ndugu waandishi wa habari mlifanya makosa kusambaza taarifa bila kuninukuu mimi ili muweze kuandika kilicho bora tofauti na kuandika vitu visivyokuwa vya kweli na askofu wa dayosisi ya Dar es Salaam bado ni mimi, hatuzitambui barua zilizosomwa katika baadhi ya makanisa,” alisema
Askofu Mokiwa alisema baada ya kikao kilichofanyika hivi karibuni katika
kanisa la ilala Dar na kuhudhuriwa na viongozi wakuu huku wakisoma
walaka wa kumvua cheo hicho mbele ya halmashauri, lakini maamuzi hayo
yaligomewa na wajumbe wa halmashauri ya Dayosisi ya Dar es Salaam.
“Ule waraka tuliupitia na kubaini kuwa hauna baraza za nyumba ya maakofu, wala hauna baraka za halmashauri ya kudumu na Sinodi ya dayosisi,” alisema na kuongeza kuwa maamuzi ya kumvua uaskofu Dk Mokiwa yamefanywa na askofu mkuu wa Tanzania kwa kushinikizwa na watu wachache aliowavua vyeo na sio vikao vya kanisa.
Lakini alipoulizwa askofu mokiwa swali na waandishi wa habari kuhusu
kudaiwa kutelekeza Nyumba iliyopo Osyterbay na nyingine iliyopo Upanga
jijini Dar alisema kuwa nyumba hizo siyo za kwake bali ni mali ya kanisa
na sio zimetelekezwa bali zipo katika hatua ya ujenzi wa nyumba za
kisasa.
Risasi liliwatafuta baadhi ya watuhumiwa waliolalamikiwa na Mokiwa kwa
kusababisha mgogoro huo ambao ni Mchungaji John Muhina wa Magomeni na
Paul Mtweve ambae alikuwa katibu wa Uinjiristi ambao kwa upande wao
kwanza walikataa kumtambua Mokiwa kama askofu tena kwani kasha vuliwa
wazifa huo.
“ Sisi ni viongozi halali wa kanisa la Anglikana Magomeni Mokiwa alitusimamisha kipindi cha uongozi wake lakini tukaamua kukata rufaa sehemu husika tukashinda.
Askofu hana uwezo wa kutuondolea uchungaji, anauwezo wa kutuvua uaskofu
laikini kikatiba tuliamua kwenda kukata rufaa katika mamlaka ya juu
ambayo yeye hana mamlka nayo ambayo ni kwa askofu Mkuu na alilidhia
rufaa yetu tukashinda,’’ alisema na kuongeza.
“Mbona yeye analalamika kuondolewa uaskofu, wakati sisi anatusimamisha alisema amefanya mabadiliko ya kawaida tu,tukakubali laikini tukaenda kukata rufaa kwenye mamlka za juu tunaona asiweke visingizio vyovyote dhidi yetu bali akubali uamuzi uliotolewa na Askofu wetu mkuu.
Post a Comment