…Diamond Platnumz.
MWEZI Januari mwaka huu katika mitandao ya kijamii aliibuka msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) aitwaye Harmonize kiasi mashabiki walimbatiza jina la ‘Pacha wa Harmonize’ au Harmorapa. Mwanzoni mwa wiki hii ameibuka msanii mwingine anayefanana na Diamond Platnumz naye kupewa jina la Chibu Rapa.
…Daimond na Chibu Rapa
…Harmonize na Harmorapa
Katika mitandao ya kijamii msanii kutoka WCB ‘Harmonize ‘ alimuanika na baadae kumtoa kijana huyo aliyefanana na Diamond huku mashabiki wakifunguka kwa kuachangia hoja na wengi walikubaliana na Harmonize kuwa ni kweli kijana huyo amefanana kwa muonekano na na Diamond Platnumz.
Aidha bado haijafahamika kama kijana huyo naye anafanya sanaa ya muziki au laa.
Post a Comment