AY (Kushoto), Mona (Kulia)
Msanii wa bongo fleva AY amewataka watayarishaji wa muziki kuwa karibu
na wasanii wao kila wanapoenda kwenye 'tour' mbalimbali ili kuweza
kujifunza mambo mengi zaidi na kuongeza ubunifu.
Akiongea kupitia eNewz AY amesema alipotoa hiyo kauli aliitoa kama wazo
lakini producer Mona Gangstar amesema yeye anawaza pesa na siyo
kuzurura na msanii ili kuongeza ufahamu wake kwa kuwa wasanii hawapendi
kulipa hela nzuri studio.
Hata hivyo Mona amemsihi AY kuwashauri wasanii wenzake kulipa vizuri
studio na AY pia amemsihi Mon kuacha kufanya kazi na wasanii ambao
hawapo tayari kumlipa pesa producer pale anapofanya kazi nzuri.
Tazama hapa video kama walivyowekwa kati kwenye eNewz
Post a Comment