Ngoma mpya ya Young Killer, Sinaga Swagga ina utata mwingi. Mmoja wa
mstari ambao tayari umeanza kumtokea puani rapper huyo ni ule usemao,
wanasema Joh anabebwa mpaka nahisi ni ukweli
Joh Makini hana jibu lenye hasira kama wengi wanavyotarajia kwasababu
kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio,
rapper huyo alisema,” Hiyo kamba, hiyo mbeleko hiyo toka 2005 mpaka
mpaka 2015 basi hiyo kamba ngumu.”
Jibu lilikuwa tofauti kwa G-Nako aliyesema, “Sometimes watu kama hawa
wanakuwa wanaongea tu kwasababu wanataka wasikike kwamba kuna vitu
wanaviongea kwenye mistari, inabidi wakifika kwenye interview kama hapa
muwe mnawachallenge, kwamba wewe umeongea hivi kwenye mistari yako,
umeshafuatilia hiki na hiki? Maake sio mistari tu.”
Kwa upande wake Nick wa Pili alisema, “tatizo ninaloliona katika mstari
kama huo ni kwamba unaharibu history sababu Joh amefanya kazi kubwa sana
so tunategemea artist wadogo si lazima kumjua Joh Makini ila kuijua
historia ya Joh Makini sababu pale ndo kuna mafunzo mengi ya kujifunza.”
Ameongeza, “Kwahiyo anavyokuja mtu akitoa neno kama hilo anaharibu ile
historia sio kwa Joh, kwa mtu ambaye anakuja mdogo. Mtu ambaye anatakiwa
kumjua Dullah hatakiwi kumjua leo, unatakiwa kujua Dullah alianzaje
kufika hapa kwasababu kila mtu anaanza moja, unaweza ukarelate na hiyo
story kikawaida.”
Joh alirejea tena kuelezea kwanini mambo kama hayo huwa hajibu akisema,
“Katika historia ya interview yangu na jinsi ambavyo nafanya kazi, huwa
sitoi nafasi kwenye vitu vya kipuuzi, navipaga tu mgongo naendelea na
mambo yangu ya msingi sababu end of the day hata nitakachosema,
hakitaleta maana sababu kama hawajui history.”
Post a Comment