0
Image result for zitto kabwe
Kupitia ukarasa wake wa Facebook amaendika haya ...Image may contain: one or more people and text
Kwanini Viongozi hudanganya?

Miaka michache iliyopita nilisoma kitabu kimoja kiitwacho WHY LEADERS LIE. Mwandishi wa kitabu hicho anaitwa John Mearsheimer. Anasema maRais husema uwongo kwa sababu huona jambo zuri kwa wananchi wao.

Hata hivyo huwezi kudanganya watu wote kwa muda wote. Unaweza kudanganya watu wachache kwa muda Fulani.

Leo Rais wetu mtukufu mpenda kusema ukweli maana msema kweli mpenzi wa mungu alikuwa huko Bariadi na kuzungumza na wananchi. Katika mazungumzo yake kasema hakuna hatari ya njaa nchini na kwamba wanasiasa na magazeti yaliyoandika kuhusu njaa wanalipwa na Wafanyabiashara wenye tani 25,000 za Mahindi bandarini. Rais wetu mtukufu anasema mahindi hayo wenye nayo wanataka yaingie nchini bila kulipa kodi, yapewe msamaha Wa kodi. Akasema mahindi hayo yametoka Brazil na ni mabovu hayafai kwa matumizi ya binaadamu. Akamalizia kwa kusema kuwa hataruhusu mahindi hayo Yaingie nchini mpaka yalipiwe kodi.

Rais wetu mtukufu anajua kuwa mahindi mabovu hayapaswi kuingizwa nchini hata Kama yakilipiwa kodi kwa sababu ni mabovu. Yanapaswa kuharibiwa na TFDA ( mamlaka ya chakula na dawa).

Rais pia amekuwa Waziri muda mrefu na anajua kuwa Tanzania kuna kitu kinaitwa pre-shipment inspection ambapo bidhaa zinazoingizwa nchini hukaguliwa huko huko zinapotoka kabla ya kuruhusiwa kupakiwa kwenye meli. Hayo mahindi mabovu yameingiaje nchini?

Rais wetu mtukufu msema Kweli mpenzi wa mungu mbona anakuwa inconsistent katika hotuba moja ndani muda mfupi? Kwa wataalamu wa saikolojia majibu wanajua. Kuna kitu Rais anaficha. Nacho ni kwamba Serikali yake ililibishia Bunge kuhusu Bajeti ya kununua chakula NFRA. Mwaka huu Serikali haikununua chakula cha akiba Ndio maana wananchi wanapata Tabu.

Hivi Serikali ina majibu ya RC wa Arusha kuhusu vibali alivyokamata vya kuuza mahindi Kenya kipindi Hiki?

Kwanini Kiongozi useme uwongo Kwa wananchi wako? Ili iwe nini? Kwanini usikiri makosa? Wakosoaji wako ndio wanaokusaidia.

Post a Comment

 
Top