0
Hakuna ubishi kuwa mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa mshambuliaji Cristiano Ronaldo katika maisha yake ya soka na anastahili kupata tuzo ambazo amekuwa akishinda kila kukicha.

Mchezaji huyo bora wa dunia kwa mara nne, usiku wa Jumatatu hii alishinda tuzo nyingine ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA na kuwabwaga wapinzani wake Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.

Ronaldo ameshindwa kuzuia furaha yake na kuamua kuweka wazi sababu ya kushinda tuzo hizo kupitia mtandao wa Twitter aliandika, “You don’t lift the trophy for best player in the world without your team. #JustDoIt.”

“Delighted to win The Best FIFA award. Wouldn’t be possible without my teammates, coaches and you who support me every day. Thanks everyone!,” ameandika katika Picha nyingine aliyoiweka katika mtandao huo.

Hii ni tuzo ya pili kubwa kushinda Ronaldo baada ya Ballon d’Or aliyoshinda mwezi Disemba kutokana na kufanya vizuri msimu uliopita.

Post a Comment

 
Top