0
Kesi hiyo iliamuliwa kwenye mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya

Uswizi imeshinda kesi kwenye mahakama ya haki ya ulaya, ambapo wazazi waislamu watahitajika kupeleka watoto wao kushirika mafunzo ya pamoja ya kuogelea.

Mahakama ilisema kuwa utawala una jukumu la kuhakikisha uwepo mfumo kamili wa masomo na kujumuishwa kwa wanafunzi.

Hata hivyo mahakama hiyo imekiri kuwa uhuru wa kuabudu umekiukwa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na raia wawili wa Uswisi wenye asili ya Uturuki ambao walikataa kuwapeleka wasichana wao kwa mafunzo ya lazima ya pamoja.

Maafisa wa elimu hata hivyo wanasema kuwa wasichana waliofikisha umri wa kubalege hawatalazimishwa kuhudhuria mafuzo hayo.

Mwaka 2010 baada ya mzozo uliodumu muda mrefu, wazazi hao waliamrishwa kulipa faini ya takriban pauni 1,100 wa kukiuka majukumu yao kama wazazi.

Walisema kuwa hatua hiyo inakiuka kipengee cha haki za bianadamu cha tume ya ulaya kinachojumuisha haki ya kuabudu.

Mahakama ilisema kuwa Uswisi ilikuwa huru kubadili mifumo yake ya elimu kuambatana na mahitaji na tamaduni.

Pia ilisema kuwa shule zina jukumu kubwa la kuwepo mchanganyiko wa kijamii.

Post a Comment

 
Top