Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Dkt.
Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7 kwa Katibu Mkuu kumaliza
changamoto zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo mkoani
Tabora.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika
hospitali ya Rufaa ya Kitete Mkoani Tabora na kukagua miradi ya chumba
cha upasuaji pamoja na Chuo cha AMOS kilichopo mkoani humo .
“Chumba hiki cha upasuaji na Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani
tangu miaka miwili iliyopita Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa
counter-part funding huku Benki ya Maendeleo ya Afrika ikiwa imetimiza
ahadi yake kwa asilimia mia moja”alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefurahishwa kutekelezwa kwa
baadhi ya maagizo aliyoyatoa kama vile kuondoa msongamano wa wagonjwa
kwenye wodi za wanawake wajawazito na watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo
umefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote muhimu na
huduma kwa wateja ikiwemo lugha nzuri kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema anashukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa
kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa na sasa hakuna
tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.
Post a Comment