Madee ndani ya FNL
Msanii wa Bongo fleva kutoka kitaa cha Manzese ambaye ndiye anayetambulika kama Rais wa Manzese, Madee, amemchana mwenzake kutoka kitaa hicho, Nay wa Mitego kwamba hana uwezo wowote kweny muziki
Madee akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV ambacho huruka LIVE kila Ijumaa Saa 3:00 usiku, aliamua kujibu mashambulizi ya Nay kwa kumrushia makombora mazito kutokana na Nay kudai kuwa ngoma mpya ya Madee ni ya kichovu na kwamba imeonesha ni jinsi gani Madee hana uwezo wa kuandika.
Katika majibu yake, Madee ambaye alikuwa akitambulisha kwa mara ya kwanza video ya ngoma hiyo ya 'Hela' alisema hata yeye haijui wala hajaisikia ngoma mpya ya Nay inayokwenda kwa jina la 'Sijiwezi' na kusema "Hiyo ngoma yake mpya siijui, wala sijaisikia maana nilikuwa nilikuwa nje muda mrefu...."
Baada ya kauli hiyo, ilibidi agongewe ngoma hiyo muda huohuo na DJ Summer ambaye ndiye aliyekuwa kwenye 'mashine', jambo la kushangaza, baada ya Madee kuisikia ngoma hiyo, aliiponda na kusema ni mbaya sana na haina hadhi ya kuimbwa na msanii mkubwa maana ni kama uchafu.
"Huo wimbo nausikia kama wa zamani sana, kama wa underground flani hivi, Sitaki kusikilizishwa tena huo uchafu" Alisema Madee
Madee alisisitiza kuwa ngoma pekee ambayo ni nzuri kutoka kwa Nay, ni
ile aliyoimba na Diamond (Muziki Gani) kwa kuwa aliimba na Diamond na
pia aliiga mawazo yake Madee.
Nay wa Mitego"Nafurahi sana nyimbo yangu ilipotoka tu siku ya kwanza akaisikia... ya kwake ya mwisho mimi kuiskia ni ile aliyoimba na Diamond, ile ndiyo nzuri, ndiyo ninayoipenda kwa sababu aliiga idea yangu ya ku'change' style"
Katika hatua nyingine, Madee alisema yuko tayari kufanya kolabo na Nay endapo atahitaji.
Huo ni mwendelezo wa vita mpya kati ya mafahari hao wawili wa manzese, iliyoanza pale Nay wa MItego aliposikilizishwa ngoma mpya ya Madee 'Hela' kupitia Planet Bongo ya EA Radio na kuiponda huku akitaka Madee asaidiwe na Rayvanny kuandika mashairi.
Post a Comment