Dkt Hamis Kigwangalla
Katika mjadala huo ambao ulikuwa ukichangiwa na watu mbalimbali, mtu mmoja ambaye anajitambulisha kwa jina la Jackline Mwaipopo alimkumbusha Dkt. Kigwangalla kuhusu ajira kwa watu wa sekta ya afya, na kwamba wao kama wataalam wa sekta hiyo hivi sasa wanalazimika kufanya kazi nyingine nje ya sekta hiyo jambo ambalo linaathiri taaluma.
Katika majibu Kigwangalla alionesha kushangazwa na mtu wa aina hiyo, yaani aliyesoma na akapata shahada, halafu anakaa kusubiri ajira za serikali na kuyaita mawazo ya aina hiyo kuwa ni ya kizamani kama inavyoonekana hapa.
"Ukitaka kufanikiwa ni lazima ukubali kuamka mapema kama na mara tu alarm yako inavyokutaka. Hii inaimarisha 'willpower' yako! Watu waliofanikiwa huamka mapema halafu Mungu, mazoezi na baadaye chai. Kila kitu kikubwa huanza na ndoto kisha imani juu ya uwezekano wake wa mafanikio halafu mpango wa utekelezaji ambao ni utekelezaji halisi. Hata siku moja usiruhusu nguvu ya woga ikaishinda nguvu ya ndoto na tamaa ya kufanikisha jambo iliyo ndani yako" Alisema Kigwangalla.
Kwa wanaotegemea kusaidiwa, (Kushikwa mkono), Kigwangalla amewaeleza "Utashikwa mkono wakati ukiwa unajaribu kupambana kupanda mlima, siyo wakati unalia lia chumbani kwako!"
Hii ni sehemu ya mjadala kuhusu siri ya mafanikio
Post a Comment