Wachezaji wa Mbeya City mazoezini
Kocha Msaidizi wa kikosi hicho Mohamed Kijuso amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanaenda vizuri na wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na kinachofanyika kwa sasa ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya kupatikana kwa ushindi wa bao 2-0.
"Tunashukuru Mungu kwa sababu tulipata matokeo kwenye mchezo wa kombe la FA licha ya mchezo kuwa mgumu, tuko mazoezini hivi sasa kurekebisha makosa yote yaliyotokea," amesema Kijuso.
Kijuso ameongeza kuwa kwa mujibu wa daktari, wachezaji wote wapo fiti kuelekea mchezo huo.
"Ninaiheshimu Tanzania Prison ni timu nzuri huwezi kuibeza kwa namna yoyote, ni wazi mchezo wa Jumamosi utakuwa mgumu," amesema Kijuso.
Kijuso ameongeza kuwa mipango na malengo ya kikosi chake ni kuhakikisha wanakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi mara ifikapo mwisho wa msimu.
Post a Comment