0
Mohamed Maulid mkazi wa Pugu Kinyamwezi ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco na mtoto wake Sumaiya Mohamed (3), wamemwagiwa mafuta ya moto na mke wake (Severine) baada ya mke huyo kupewa talaka siku mbili kabla ya tukio hilo.

Maulid alisema baada ya kumpa mwanamke huyo talaka alikuwa anampiga tu tarehe kuwa ‘ntaondoka kesho, ntaondoka kesho.’ “Na nilivyokuwa naenda kazini nilimuuliza utaondoka saa ngapi akasema ataondoka jioni, nikahisi kwamba anaona aibu kuondoka mchana ataondoka jioni,” amesimulia.

“Nilikuwa nimelala nikasikia kama moto umelipuka, nilikuwa nimelala fofoFo, nikashtuka nikaanza kupiga kelele nimemwagiwa maji ya moto nikapiga kelele majirani wengine wakanisikia wakatoka nje, wakaenda kumuangalia na mtoto wakakuta na mtoto naye kaungua sana na yupo kule wodi ya watoto.”

Baadaye majirani wakanisaidia wakamuita dereva taksi nikawaambia nikimbizeni hospitali kwa uzima wangu. Mimi nilipomwagiwa mafuta yale, nilikurupuka nikakuta mlango upo wazi na wakati mlango nilikuwa nimefunga nimefunga na misumari kwasababu nilikuwa simuamini tena kwanini hataki kuondoka, nikakuta mlango ule umefunguliwa na wa nyuma umefunguliwa na mtoto wangu alimwagiwa mafuta kichwani nilimuona.”

Jirani yao aliyejulikana kwa jina la Sofia Ngumbali alisema, “usiku mwanamke huyo alienda jikoni kuchemsha mafuta na akapanga viti akarukia chumba cha mumewe kufika pale mlangoni kwa kuwa funguo alikuwa hajaichomoa akafungua mlango na akachukua mafuta akaja kuwamwagia yeye na mwanae waliokuwa wamelala pamoja.”

“Yule mwanaume alivyokurupuka akapiga kelele majirani tulijua mwizi kukurupuka tukamkuta anagalagala nje anasema kuwa mkewe amemmwagia mafuta, na sisi tulikuwa tunaona wanaishi kwa amani wakitoka wanatoka wote na kurudi wote kwahiyo ya ndani mtu huwezi kujua yaliyopo ndani ya ndoa,” aliongeza jirani huyo.

Kwa upande wake mama wa mtuhumiwa huyo akiwa na mjukuu wake katika hospitali hiyo aligoma kutoa ushirikiano alipokuwa akihojiwa na waandishi.

Post a Comment

 
Top