0
AY kwa maneno yake mwenyewe, si mtu anayependa kufanya kitu kile kile muda wote akitarajia matokeo makubwa.

Amesema kwa sasa ameamua kupita njia tofauti ikiwemo kurudisha strategy za muziki wa zamani, ambapo msanii alikuwa akiweka nguvu zote kwenye audio kwanza, bila kutarajia kuwa video itambeba.

Ameiambia Bongo5 kuwa, miaka ya hivi karibuni kufuatia mapinduzi ya video za gharama, ambayo kimsingi yeye ndiye alikuwa muasisi, wasanii wengi wamekuwa wakiumiza vichwa zaidi kufanya video kubwa na wengine bila kuzingatia sana uzito wa audio yake. Hicho ni kitu anasema kwa sasa hakizingatii tena.

“Siku hizi watu wanajaji ngoma kwa video kuliko audio. Kwahiyo sasa hivi najaribu kurudi kule kwa 2008 kurudi nyuma, vile ambavyo tulikuwa tunafanya zamani,” AY ameiambia Bongo5.

“Nataka kuirudisha ile strategy ya zamani, ili watu waconcentrate zaidi kwenye audio, yaani unaenda kwenye redio watu hawasifii audio wanasifia video zaidi. Fanya audio iwe kali halafu unafanya video kali,” amesisititiza.

Hivi karibuni AY aliachia single mpya iitwayo More & More aliyomshirikisha Nyashinski.

Post a Comment

 
Top