0
ais mpya wa Gambia Adama Barrow, amewasili nchini humo kuchukua hatamu za uongozi, kufuatia kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya JammehBarrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani.

Maelfu ya watu walifurika katika barabara za mji mkuu wa Gambia Banjul kumlaki rais huyo mpya.
Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Post a Comment

 
Top