Rais Magufuli
Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi
wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu bwana Gerson
Msigwa imesema "Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu
wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwana Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye."
Taarifa za kujiuzulu kwa Mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana
zikidai kuwa Mkuu huyo wa Wilaya aliaga katika Kamati ya Madiwani wa
CCm, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa halmashauri kuwa ameamua
kuchia ngazi, bila kueleza sababu sababu za uamuzi huo.
Hata hivyo baadaye kulitokea utata baada ya kusambaa kwa taarifa za yeye
kukanusha kufanya uamuzi huo, lakini sasa ni dhahiri kuwa Bw. Gabriel
Simon Mnyele siyo mkuu wa wilaya hiyo ten
Post a Comment