Watu wanne wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa Mtwara
Watu wanne wamefariki dunia hapo hapo huku wengine 22 wakijeruhiwa
katika ajali iliyohusisha gari aina ya Tata yenye namba za usajili T 390
DEQ iliyokuwa inatokea kijiji cha Maundo wilayani Tandahimba, mkoani
Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na ITV baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya
Nyangao wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva.
Kwa upande wake muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Nyangao, Edgar
Chilemba,amekili kupokea miili ya marehemu wanne pamoja na majeruhi 22
ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
ITV ilimtafuta kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Renata
Nzinga lakini simu yake ilipokelewa na mlinzi wake na kusema bosi wake
yuko kwenye kikao.
Post a Comment