0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjibu Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora aliyeomba kujiuzulu wadhifa huo.

Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa imesema

"Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye."

Taarifa za kujiuzulu kwa mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana zikidai kuwa aliaga katika Kamati ya Madiwani wa CCM na kamati ya siasa ya wilaya, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kuwa ameamua kuachia ngazi, bila kueleza sababu za uamuzi huo.

Post a Comment

 
Top