Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaua watu wawili wanaodaiwa
kuwa ni majambazi na kukamata silaha pamoja na watuhumiwa kadhaa wa
matukio ya kihalifu wakiwemo 7 wanaotuhumiwa kutengeneza kadi 7 za
bandia za chanjo ya homa ya manjano
Akizungumza na vyombo vya habari, jana Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro alisema,
mnamo tarehe 23 mwezi wa kwanza mwaka 2017 majambazi hao walitekeleza
tukio la mauaji na kupora kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 3 huko
Boko Basihaya na polisi iliwasaka na kuwakamata na wakakiri kutenda
mauaji hayo na kwamba walipojaribu kutoroka ndipo walipouawa.
Akielezea
kukamatwa kwa watu 7 wanaodaiwa kutengeneza kadi bandia za homa ya
manjano ambazo mtu hupaswa kuchomwa chanjo hiyo kabla ya kusafiri nje ya
nchi, Kamisha Sirro alisema, watu hao wamekuwa wakitoa kadi hizo na kudai fedha nyingi kinyume cha sheria.
Kamanda Sirro akionesha mkasi unaotumiwa na wahalifu kuvunja vitu mbalimbali
Jeshi
hilo pia limewakamata watuhumiwa 92 wa makosa mbalimbali, ikiwemo wizi
wa magari na pikipiki, watengenezaji wa gongo, shisha na uuzaji wa
bangi.
Pia limekusanya zaidi ya Shilingi milioni 918, kwa ukamataji wa makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha siku 10.
Kamanda Sirro akionesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment