Rais wa Mexico akiwa na Rais Mteule wa Marekani |
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesisitiza kwa mara nyengine kwamba nchi yake haitalipia ukuta katika mpaka na Marekani.
Ametoa kauli hiyo baada ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kusema
katika mkutano wake na waandishi wa habari kwamba anataka kuanza
kuujenga haraka na kwamba Mexico itailipa Marekani kwa gharama
iliyoingia.
Bwana Pena Nieto amewaambia wanadiplomasia wa kigeni kwamba yuko tayari
kujadili mustakbali wa makubaliano ya kibiashara ya Kaskazini ya
Marekani, ambapo Trump amesema hayo ni makubaliano mabaya ya kibiashara
kuwahi kupitishwa na Marekani.
Post a Comment