Huku
raia wa Marekani wakitizama hotuba ya mwisho ya rais Obama mjini
Chicago siku ya Jumanne usiku, wengine waliwachwa na swala moja.
Sasha Obama alikuwa wapi?. Picha ya kwaheri iliopigwa ilimuonyesha Obama
,mkewe na mwanawe mkubwa Malia mbele ya jukwaa, lakini msichana hyo wa
miaka 15 hakuonekana.
Imeelezewa kwamba msichana huyo alikuwa akifanya mtihani katika shule ya Sidwell mapema siku ya Jumatano.
Shule hiyo ndio imewafunza wana wa marais kwa miaka mingi akiwemo Chelsea Clinton.
Ujumbe wa Twitter uliotumwa na baadhi ya raia nchini Marekani wakitaka kujua Sasha aliko
Kwa hivyo imekuwa ikitumika kukabiliana na wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa darasa kutokana na kuhudhuria maswala ya uongozi.
Lakini hilo halikusitisha kuanzishwa kwa #WhereIsSasha katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya watu walitarajia kwamba anajaribu kumzuia Donald Trump kuingia ikulu ya Whitehouse.
Post a Comment