Dar es Salaam. Jeshi la polisi limepiga marufuku uuzaji wa silaha za
jadi kama panga, mishale, manati, visu pembezoni mwa barabara nyakati za
foleni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum
Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwekuwa na vitendo vya kialifu
vikifanyika kwa baadhi ya wafanyabiashara hao pia ni hatari kwa hali ya
usalama wa wananchi.
“Biashara hii imeshamiri kwa kasi katika barabara ya Nyerere, Tazara na
kwenye mataa ya Chang’ombe na Gerezani huwa wanawaibia watu kwenye
magari binafsi na umma vitu kama pochi, kompyuta mpakato, saa na simu za
mikononi,” amesema Sirro.
Sirro amesema tayari jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja na Mgoli S/O Sakalani (39) mkazi wa
Banana, Ilala na mtu yoyote atakayetaka kufanya biashara hiyo ni lazima
kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo na anatakiwa kuwa na eneo
maaulum litakalotambulika kisheria.
Post a Comment